MTOTO WA MWAKA MMOJA ACHOMWA MOTO WEST BANK

Mtoto wa mwaka moja achomwa moto West Bank
Mtoto mchanga wa kipalestina ameuawa baada ya nyumba yao kumwagiwa petroli na kuchomwa moto katika makazi ya West Bank.

Walioshuhudiwa wanawashuku walowezi wa kiyahudi kuwa ndio waliotekeleza shambulizi hilo.
Yamkini mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na u nusu alikuwa ndani ya nyumba yao ilipomwagiwa petroli na kuchomwa.
Nyumba yao iliyoko katika kijiji cha Duma Kusini mwa Nablus inaaminika ililengwa maksudi na walowezi wa kiyahudi.
Serikali ya Israeili imetaja mauaji hayo kuwa ya ''kigaidi''.
Wazazi wake na kakake walinusurika shambulizi hilo ambalo serikali ya Israeili imeitaja kuwa ya ''kigaidi''.
Wenyeji wa kijiji hicho cha Duma wanasema waliotekeleza shambulizi hilo waliandika ''kisasi'' kwenye ukuta wa vifusi vya nyumba hiyo pamoja na ishara ya nyota ya daudi

Comments