AL SHABAAB WAKUBALI KUHUSIKA NA SHAMBULIZI LA KENYA
Wanamgambo wa Al Shabaab wamesema
kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi Kaskazini Mashariki mwa Kenya
ambapo watu 14 waliuawa usiku wa kuamkia jumanne.
Shambulio hilo linaaminika kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokua wenyeji wa mkoa huo.
Walioshuhudia wameambia BBC kuwa walisikia mwanzo milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio ya risasi.
Shirika la msalaba mwekundu linaongoza oparesheni ya kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani .
Nani washambuliaji ?
Wanamgambo wa Al shabaab wamekuwa wakilenga wakaazi wasio wenyeji wa asili katika eneo hilo katika mashambulio yaliyotangulia.
Shambulio
kama hilo dhidi ya wachimba migodi lilitokea jijini Mandera mwezi
Disemba 2014, ambapo takriban watu 36 waliuawa na wengine wengi
kujeruhiwa.
Marudio ya shambulio
Mashambulio
kama haya yametishia kudumaza shughuli za maendeleo na kiuchumi katika
eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake
ni watu kutoka maeneo mingine ya Kenya.
Wafanyikazi hawa wamekuwa
wakidai kutishiwa maisha, na wengi wa wafanyikazi kama vile walimu na
hata wahudumu wa afya wamesusia kurejea kazini katika eneo hilo wakidai
kutishiwa maisha yao.
Chini ya siku kumi zilizopita serikali ya
Kenya iliondoa marufuku ya kutoka nje kuanzia magharibi hadi alfajiri,
kufuatia wito kutoka kwa viongozi wa kiislamu waliodai kuwa marufuku
hiyo inahujumu ibada za waislamu za usiku katika mwezi wa Ramadhani.
Asili mia kubwa ya wakaazi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya, ni waislamu wa asili ya kisomali.

Comments
Post a Comment