ARTUDO VIDAL ANUSURIKA KWENDA JELA

VIDAL AKIWA MAHAKAMANI
Nyota wa Chile, Arturo Vidal amenusurika kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa. Lakini mahakama ya San Bernardo karibu na jiji la Santiago, Chile ikapunguza makali ya adhabu hiyo.




Alisababisha ajali hiyo siku kadhaa kabla ya michuano ya Copa America akiwa na gari lake la kifahari aina ya Ferrari.

Vidal aliyeiongoza Chile kubeba ubingwa wa Copa America, amepunguziwa adhabu na sasa ametakiwa kulipa hasara alizowasababishia madereva wa magari mengine aliyoyagonga.

Baada ya hapo, amepewa adhabu nyingine ya kwenda kutoa hutoba ya onyo na kuwapa matumaini wafungwa walio gerezani.

Pia ameahidi kununua vifaa mbalimbali vya michezo kwa watoto na jamii.

AKIONDOKA MAHAKAMANI


Kabla ya hapo, Vidal anayekipiga Juventus ya Italia pia aliomba radhi kutokana na kuwadhalilisha askari polisi waliomkamata.

Comments