AZAM KUJIONGEZA
Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' anakuja Jumatano kumalizana na Azam FC |
KIUNGO
wa kimataifa wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' anatarajiwa
kutua nchini Jumatano kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuichezea Azam FC.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu ya Azam, Saad Kawemba ameiambia KAKWAYA100 leo kwamba mazungumzo ya awali na mchezaji huyo yamekwishafanyika na wamefikia pazuri.
"Baada ya kutua tutakamilisha mazungumzo na Nahodha huyo kwa ajili ya kuanza kumtumia katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa,"amesema Kawemba.
Awali APR ilikubali kumuuza mchezaji huyo baada ya kumalizika kwa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) lakini sasa tayari imemruhusu kuja nchini kujiunga na Azam.
Adha, Kawemba amesema kwamba katika kujiandaa na mashindano ya Kombe la Kagame, kesho timu yao itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kawemba amesema baada ya mchezo huo, kikosi kitawasili hadi Tanga Jumamosi kwa mechi mbili zaidi za kujipima dhidi ya African Sports na Jumapili dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.

Comments
Post a Comment