BENITEZ AANZA KAZI RASMI MADRID

 
Kocha Rafa Benitez, rasmi ameanza kazi yake mpya katika kikosi cha Real Madrid.

Benitez ameonekana ofisini akiwa katika mipango kwa ajili ya msimu mpya.
Kocha huyo aliyechukua nafasi ya Carlo Ancelotti, pia alifanya ziara mara kadhaa kwenye viwanja vya timu hiyo.

Utamaduni wa Madrid, kocha kila msimu lazima achukue angalau kikombe kimoja, akikosa, safari inamkuta, hakuna mjadala.

Comments