DAWA INAYOPUNGUZA MAKALI YA SARATANI YA MATITI
Dawa inayouzwa kwa bei rahisi na
ilio salama inaweza kuwasaidia nusu ya wanawake walio na saratani ya
matiti kuishi kwa muda mrefu wanasayansi wanasema.
Utafiti huo
uliochapishwa katika jarida la asili,uko katika awamu ya kwanza lakini
homoni za Progesterone zinaweza kutumika kupunguza ukuwaji wa uvimbe
.
Watafaiti hao kutoka nchini Uingereza na Australia wanasema kuwa matokeo hayo ni muhimu na sasa wanaanda majaribio yake.
Utafiti wa saratani nchini Uingereza unasema kuwa utafiti huo ni muhimu sana na unaweza kuwasaidia maelfu ya wanawake.
Homoni huchangia pakubwa katika saratani ya matiti.
Zinaweza
kuigawanya seli ilio na saratani kupitia kukutana na seli inayoweza
kutoa ishara katika sehemu ilioathirika na saratani.
Ufanisi mkuu wa dawa hiyo ya
saratani,tamoxifen ni kukabili homoni ya oestrogen.Saratani yenye seli
za homoni ya progesterone haina madhara makubwa.
Na sasa kundi
moja la watafiti katika chuo kikuu cha Cambridge pamoja na kile cha
Adelaide wametafiti kuhusu seli za saratani zinazokuwa katika maabara.
Zinaonyesha
kuwa seli zenye homoni za progesterone pamoja na oestrogen zina
uhusiano wa karibu na kwamba seli hizo za homoni ya progesterone
zinaweza kupunguza madhara yanayosababishwa na seli za oestrogen.
Seli za saratani zinazokuwa
katika maabaara zilikuwa nusu yake zilipotibiwa na progesterone na dawa
ya tamoxifen ikilinganishwa na dawa ya tamoxifen pekee.
Mmoja wa
watafiti ,profesa Carlos Caldas kutoka chuo kikuu cha Cambridge
ameiambia BBC :inaonekana kwamba unaweza kudhibiti uvimbe huo
vizuri,lakini ili kubaini iwapo inafanya kazi vyema miongoni mwa
wanawake walio na saratani ya matiti ni lazima tuifanyie majaribio.
Watafiti hao wako katika awamu ya kwanza ya kuandaa majaribio.
Asilimia 75 ya wanawake wana
saratani ya matiti ilio na seli zilizo na homoni za Oestrogen na
vilevile asilimia hiyo pia ina seli zenye homini za Progesterone
Comments
Post a Comment