DE GEA AIKANA MADRID

KIPA David de Gea atarejea Manchester United kwa maandalizi ya msimu mpya atakapomaliza mapumziko yake mjini Madrid.
KIpa huyo wa kimataifa wa Hispania, anatarajiwa kusaini Real Madrid kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuwaambia wachezaji wake juu ya dhamira ya kuondoka Old Trafford.
Alishindwa kujibu ofa ya mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki, lakini hataondoka kabla ya United kuanza matayarisho ya msimu mpya wiki ijayo.

David de Gea ameliambia gazeti la Cuatro kwamba atarejea mazoezini Manchester United kujiandaa na msimu mpya

Lakini De Gea ameliambia gazeti la Cuatro: "Real Madrid? Natakiwa kurejea Manchester kwa maandalizi ya msimu," alisema baada ya kugoma kujibu maswali kadhaa juu ya mustakabali wake.
Pia amekiri ametulia kwa sasa akiangalia mambo yanavyokwenda kuhusu mustakabali wake kwa sasa licha ya uvumi wa kuhama.
Van Gaal anatarajiwa kuwa na mazungumzo na De Gea wiki ijayo wakati wote wakijaribu kutafuta suluhisho, huku mchezaji huyo akiwa katika mwaka wa mwisho wa Mkataba wake.

Comments