JAMES MILNER APEWA JEZI NAMBA 7 LIVERPOOL
KIUNGO
James Milner ametambulishwa kama mchezaji wa Liverpool leo na kusema
kiu yake ni kushinda mataji na Medali kibao akicheza dimba la kati
Anfield.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa England amesema anataka kuendeleza desturi ya
kuinua mataji kama ilivyokuwa Manchester City baada ya kupata nafasi ya
kufanya kazi na kocha Brendan Rodgers.
Ingawa
hakusema moja kwa moja kuhusu Steven Gerrard baada ya kukabidhiwa jezi
namba 7, Milner alisema pengo lililoachwa na gwiji wa Liverpool
halitasumbua.
James Milner ametambulishwa leo Liverpool na kusema anataka kushinda mataji na Medali Anfield
Kiungo huyo wa kimataifa wa England amepewa jezi namba 7 Liverpool baada ya kusajiliwa kutoka Manchester City
Comments
Post a Comment