KAPTENI CAMARA ASHTAKIWA RASMI HUKO GUINEA
wa serikali Guinea
wamemshataki rasmi aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini humo Moussa Dadis
Camara kuhusu mauaji ya halaiki yaliotokea katika uwanja wa michezo
kwenye mji mkuu mnamo 2009.
Wanajeshi nchini humo wanashutumiwa kwa kuawaua watu 150.
Kapteni Camara alishtakiwa huko Burkina Faso anakoishi uhamishoni tangu alipojiuzulu urais.
Kiongozi huyo wa zamani wa Junta alinyakua madaraka kupitia mapinduzi 2008.
Mashtaka hayo hayajabainishwa
wazi lakini Kapteni Dadis Camara alihojiwa kuhusu tuhuma hizo za
kuhusika katika mauaji hayo ya halaiki.
Takriban watu 157 waliuawa
wakati vikosi vya usalama vilifyetua risasi dhidi ya kundi la
waandamanaji waliopinga kugombea kwake urais katika uchaguzi mkuu
nchini.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema wanawake wapatao 1000 pia walibakwa.
Jitihada
za kumshtaki zilianza 2010 na mahakimu wanaoiongoza kesi hiyo
waliwahoji mamia ya waathiriwa, lakini kesi hiyo bado inatarajiwa
kusikizwa.
Chama cha kisiasa cha Camara kimetaja kuwasilishwa
rasmi kwa mashtaka dhidi ya mkuu huyo wa jeshi wa zamani kama siasa
tupu, na hatua ya kumzuia kugombea urais katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa baadaye mwaka huu.
Comments
Post a Comment