KIKOSI CHA CHILE WAINGIZA KOMBE IKULU
KIKOSI cha Chile kimetinga Ikulu kumuonyesha Kombe la Copa America Rais Michelle Bachelet na kushreheeka naye baada ya usiku wa penalti 4-1 dhidi ya Argentina usiku wa kuamkia leo.
Mshambuliaji
wa Arsenal, Alexis Sanchez alifunga penalti ya ushindi Uwanja wa Taifa
mjini Santiago na Chile ikaripuka kwa shangwe za ubingwa wa Copa America
2015..
Saa kadhaa baada ya ushindi huo, wachezaji wote wakazuru Ikulu La Moneda mjini Santiago kupewa hongera zao na Rais Bachelet.
Maelfu ya wananchi wa Chile walijimwaga mitaani kusherehekea ushindi huo wakati pati la Rais na wachezaji likendelea Ikulu.
Rais Bachelet akiinua Kombe la Copa America Ikulu leo
Comments
Post a Comment