KUMBU KUMBU LA SHAMBILIZI LA KIGAIDI YAFANYIKA LEO HUKO LONDON
Raia wa Uingereza leo wameadhimisha mia kumi tangu shambulio la kigaidi katika kituo kimoja cha treni.
Watu 52 waliuawa katika shambulizi hilo lililotekelezwa na kundi la waislamu wenye msimamo mkali.
Maafisa wa uokozi na familia ya wahasiriwa walihudhuria misa maalum katika kanisa la mtakatifu Paulo mjini London.
Mabomu
manne yalilipuka, wakati wa shambulio hilo, matatu yakiwa yametegwa
ndani ya treni inayotumia barabara za chini ya ardhi na nyingine kwenye
basi moja la abiria.
Wakati wa hafla hiyo Cameron alisema kuwa Uingereza haiwezi kutishwa na Ugaidi.
Na katika tangazo ambalo
halikutarajiwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi MI5 Andrew Parker
amesema maafisa wake wanafanya kila juhudi ili kuzuia kile alichokitaja
kama changamoto kuu inayokumba taifa hilo.
Bwana Parker amesem akuwa idara yake inafanya kila iwezalo kuwalinda waingereza
Bwana
Cameron amesema kuwa mauaji ya waingereza zaidi ya thelathini nchini
Tunisia ni kama ukumbusho wa kutisha kuwa ugaidi upo na unaweza kutokea
wakati wowote.
Comments
Post a Comment