MAN UNITED YAENDEREA KUIMALISHA UKUTA WAKE YAMSAINISHA BEKI MATTEO DARMIAN
BEKI Matteo Darmian atasaini Manchester United baada ya kukubali Mkataba wa miaka minne.
United
imekubai kutoa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 12.7 kwa Torino, ambayo
inaweza kuongezeka hadi Pauni Milioni 14.4 iwapoa mchezaji huyo
atafanya vizuri.
Klabu ya kwanza ya Darmian, AC Milan pia inatarajiwa kupata Pauni 287,000 kama sehemu ya asilimia tano yao kwa mauzo ya mchezaji huyo.
Matteo Darmian akiichezea Italia katika mechi ya kufuzu Euro 2016 dhidi ya Bulgaria Machi, mwaka huu
Taratibu
za mwisho zilitarajiwa kukamilishwa jana baina ya wanasheria wa pande
zote na mchezaji huyo anatarajiwa kutangazwa rasmi leo.
Bei
huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25, anayeweza kucheza
kulia na katikati atakuwa mchezaji wa pili kusajiiwa United kuelekea
msimu ujao, baada ya Memphis Depay kutoka PSV Eindhoven.
Depay atatambulishwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kesho.United inahitaji mchezaji anayeweza kucheza kulia baada ya Louis van Gaal kuona Mbrazili, Rafael hawezi kazi hiyo.
Comments
Post a Comment