MAYWEATHER APOKONYWA TAJI ALILOMSHINDA PACQUIAO

 
Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa aliyopewa ya tarehe 3 Julai.
Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.
Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama mshikilizi wa taji hilo.
null
Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei
Taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.
Yamkini Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao,angevua mataji yote ya vijana ilikuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.
Taarifa yao iliyochapishwa katika mtandao wa wboboxing.comimesema kuwa ''hatukukuwa na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu.kwa hivyo hatutamtambua mayweather kama mshikilizi wa ukanda huo wa Welter''
Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
null Hata hivyo Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.
Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la welter linalopangwa kufanyika tarehe 27 kati ya Bradley na Jessie VargasA

Comments