MBABAZI NA BESIGYE WAZUIWA NA POLISI UGANDA
Wagombea wawili wa urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka Ujao Uganda wamezuiwa na Polisi katika sehemu tofauti.
Aliyekuwa
waziri mkuu Amama Mbabazi alikamatwa na polisi akiwa mjini Jinja mwendo
wa saa moja kutoka jijini Kampala, akiwa njiani kuelekea mkutano wake
wa kwanza wa hadhara na wafuasi wake mjini Mbale mashariki mwa nchi.
Siku
ya Jumatano Polisi nchini Uganda walitoa taarifa kusema kuwa bwana
Mbabazi hana ruhusa ya kufanya mikutano yoyote ya kisiasa japo alikuwa
amewataarifu.
Bwana Mbabazi ananuia kutafuta uteuzi wa chama
kinachotawala NRM kuwa mgombea wake rasmi wa Urais katika uchaguzi huo
Machi mwaka ujao.
Kwa upande mwingine wa nchi
mwansiasa mwingine wa Upinzani Kizza Besigye alikamatwa na polisi akiwa
nyumbani kwake. Dr. Besigye , ambaye ni kanali mstaafu wa jeshi amewahi
kuwania urais wa nchi hiyo mara tatu bila mafanikio.
Alikamatwa akiwa njiani kwenda kwa mkutano wake wa kwanza na wafuasi wa chama chake cha Forum For Democratic Change.
Msaidizi
wa Dr Besigye ameambia BBC kuwa mwanasiasa huyo anazuiliwa katika kituo
cha polisi karibu na nyumbani kwake. Besigye anashindania kiti hicho
cha FDC na aliyekuwa kamanda wa jeshi Gen. Mugisha Muntu.
Dr.
Besigye pamoja na bwana Mbabazi wote walikuwa washirika wa karibu zaidi
na rais Yowei Museveni ambaye atashindana nao katik auchagzui
huo.Museveni amekuwa uongozini kwa miaka thelathini.
Kwa sasa #FreeBesigye
inaendelea kutajwa kwa wingi katika mitandao ya kijamii, baada ya watu
kugeukia mitandao hiyo kuelezea hisia zao kuhusu kukamtwa kwa wawili hao
- Saa 4 zilizopita

Comments
Post a Comment