MESSI,RONALDO NA WENGINE AMBAO WALIWIKA KLABUNI KWAO ILA HAWANA MSAADA KWENYE MATAIFA YAO
NI
Lionel Messi mwenye pekee anajua kilichokuwa kwenye mawazo yake wakati
mashabiki wadogo walipomfuata kuomba kupiga naye picha katikati ya
Uwanja mjini Santiago, muda mfupi baada ya Argentina kushindwa kumaliza
ukame wa mataji wa miaka 22.
Kwa bahati mbaya, nyota huyo wa Barcelona, alisimama kupiga picha na kuwasainia hiyo ikiwa sehemu ya wajibu wake kama mchezaji mkubwa, hata baada ya ndodo zake kuyeyuka.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 anaweza assinue tena taji akiwa na timu
yake ya taifa ya Argentina hadi anastaafu, tangu ashinde Medali ya
Dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008 China.
Mshindi
huyo mara nne wa Ballon d'Or si mchezaji pekee mkubwa ambaye alistaafu
bila kushinda taji na timu yake ya taifa. Hapa, BIN ZUBEIRY SPORTS inakueletea wachezaji 10 wakubwa ambao hawajashinda mataji na timu zao taifa.
Lionel
Messi akiwa mnyonge baada ya Argentina kufungwa katika fainali na Chile
kwa penalti 4-1 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120
Johan Cruyff, Uholanzi (1966-77: Mechi 48, mabao 33)
Alishinda
mataji mfululizo na klabu za Ajax, Barcelona na Feyenoord, lakini
hakuna hata moja alilotwaa akiwa na jezi ya Uholanzi. Katika ngazi ya
klabu, ameshinda mataji 10 ya Eredivisie na La Liga, na matatu ya Ulaya.
Mafanikio
makubwa kwa gwiji huyo kwenye soka ya kimataifa ni nafasi ya pili
katika Kombe la Dunia Ujerumani mwaka 1974, taji ambalo lilichukuliwa na
wenyeji na kushika nafasi ya tatu katika Euro mwaka 1976Yugoslavia.
Johan Cruyff alishinda mataji kibao akiwa na Ajax, Barcelona na Feyenoord, lakini hakushinda na Uholanzi
Ferenc Puskas, Hungary (1945-55: Mechi 85, mabao 84), Hispania (1961-62: Mechi 4, hakufunga)
Hungary
ilitawala ulimwengu wa soka mwanzoni mwa miaka ya 1950. Puskas, kama
Messi, alishinda Medali ya Dhahabu ya Olimpiki mwaka 1952, na
hawakufungwa ndani ya miaka minne hadi wanafika katika Kombe la Dunia
mwaka 1954.
Walifika fainali, ambako Puskas alifunga bao la kuongoza licha ya kucheza amefungwa kichwani baada ya kupasuka.
Hungary iliongoza 2-0, lakini mwishowe ikafungwa 3-2 na Ujerumani Magharibi.
Ferenc Puskas aliichezea Hungary kati ya 1945 na 1955 mechi 85 na kufunga mabao 84
Eusebio, Ureno (1961-73: Mechi 64, mabao 41)
Mmoja kati ya wachezaji wakubwa kwa uwezo binafsi aliyeshinda mataji 11 na moja la Ulaya akiwa na Benfica.
Mafanikio makubwa katika soka ya kimataifa kwa mshindi huyo wa Ballon d'Or 1965 ni mwaka 1966, alipoiwezesha Ureno kumaliza nafasi ya tatu Kombe la Dunia.
Ureno
kwa ujumla hawakuwa na timu bora ya kushinda Kombe hilo mwaka huo na
Eusebio alijitolea kwa uwezo wake wote wote, lakini wapi!
Eusebio alikuwa mmoja wachezaji bora mno wenye uwezo binafasi na akashinda mataji 11 na moja la Ulaya akiwa na Benfica
Zico, Brazil (1976-86: Mechi 71, mabao 48)
Tuzo
binafasi alizoshinda Zico ni lukuki. Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji
bora duniani mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980,
ambayo Pele anakiri, lakini CV yake haijakamilika.
Zico alishinda nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia mwaka 1978 na akafika Robo Fainali mwaka 1986, lakini hakuwahi kutwaa taji.
Zico alishinda nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia mwaka 1978 na Robo Faibali mwaka 1986
Paolo Maldini, Italia (1988-2002: Mechi 126, mabao 7)
Maldini
ameshinda mataji ya Serie A akiwa na AC Milan, pamoja na mataji matano
ya Ulaya. Lakini anapokuwa na jezi ya Italia, beki huyo hana cha
kujivunia.
Nafasi
ya pili katika Kombe la Dunia mwaka 1994 na Euro 2000, nafasi ya tatu
katika Kombe la Dunia mwaka 1990, na Nusu Fainali Euro 1988 ndiyo
mafanikio makubwa kwa Maldini
kwenye soka ya kimataifa kabla ya kustaafu akiwa ana umri wa miaka 34
baada ya Kombe la Dunia mwaka 2002, miaka minne kabla ya Italia kutwaa
taji hilo nchini Ujerumani mwaka 2006.
Paolo Maldini ameshinda mataji saba ya Serie A akiwa na AC Milan, lakini hajashinda chochote na Italia
Roberto Baggio, Italia (1988-2004: Mechi 56, mabao 27)
Gwiji
mwingine wa Italia, ambaye aliisaidia nchi yake kufika fainali ya Kombe
la Dunia mwaka 1994 tena akiwa mfungaji bora wa mashindano.
Baada
ya sare ya 0-0 na Brazil ndani ya dakik 120, Baggio alikwenda kukosa
penalti ya mwisho na akashindwa kutimiza ndoto za kubeba Kombe la Dunia.
Roberto Baggio alikosa penalti ya mwisho katika Kombe la Dunia mwaka 1994 dhidi ya Brazil
Michael Ballack, Ujerumani (1999-2010: Mechi 98, mabao 42)
Ballack
aliifikisha Ujerumani fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002, lakini kadi
ya njano aliyopewa kwa faulo ya kijanja aliyocheza katika Nusu Fainali
dhidi ya Korea Kusini ilimfanya aukose mchezo wa fainali dhidi ya
Brazil.
Ujerumani
ilifungwa 2-0 na Brazil. Alikuwepo kwenye kikosi cha Ujerumani
kilichofika fainali Euro 2008 akiwa Nahodha wakifungwa na Hispania.
Pamoja
na kutamba akiwa na klabu za Bayer Leverkusen, Bayern Munich na
Chelsea, lakini Ballack hakuwahi kutwaa taji akiwa na Ujerumani.
Michael Ballack hakushinda taji lolote akiwa na Ujerumani licha ya kuichezea kwa miaka 11
Paul Gascoigne, England (1988-98: Mechi 57, mabao 10)
Kweli,
unaweza kusema wakali wa England kama David Beckham, Steven Gerrard,
Frank Lampard, Paul Scholes hawana nafasi hapa, lakini Gazza anastahili
kuwamo kutokana na machozi aliyomwaga Italia '90.
Ni
huko ambako England ilimaliza katika nafasi ya nne na Gascoigne
alimwaga machozi baada ya kuonyeshwa kadi ya njano dhidi ya Ujerumani
Magharibi katika Nusu Fainali, maana yake angekosa fainali hata kama
wameshinda.
Paul Gascoigne alimwaga machozi Italia '90 wakati England ikifungwa na Ujerumani Magharibi katika Nusu Fainali
Michael Laudrup, Denmark (1982-98: Mechi 104, mabao 37)
Wengi
wanaamini Laudrup wa miaka 1990 ni kama Cruyff wa miaka ya 1970.
Laudrup alikuwa nyota babu kubwa, aliyeshinda mataji na Juventus,
Barcelona, Real Madrid na Ajax.
Lakini
hakuwa kushinda taji lolote na Denmark. Walifuzu kutoka Kundi E Kombe
la Dunia mwaka 1986, lakini wakatolewa kwa kufungwa mabao 5-1 na
Hispania katika raundi iliyofuata.
Na wakati Denmark wanatwaa taji la Euro 1992, Laudrup alikuwa tayari amestaafu soka ya kimataifa waakti wa mechi za kufuzu.
Kocha wa zamani wa Swansea City, Michael Laudrup hakuwahi kushinda taji na Denmark
Brian Laudrup alishinda Euro 1992 akiwa na Denmark, lakini kaka yake, Michael hakucheza mashindano hayo
Cristiano Ronaldo, Ureno (2003- hadi sasa: Mechi 120, mabao 55)
Muda unayoyoma na akiwa na umri wa miaka 30 sasa, Cristiano Ronaldo anaelekea kustaafu soka ya kimataifa bila taji.
Ronaldo hawezi hatasahau Euro 2004 ambayo Ugiriki iliifunga Ureno kutwaa taji hilo kama wenyeji. Je, kati yake na Messi katika umri wa miaka 30 na 28 mmoja wao au wote wanaweza kutimiza ndoto zao siku zijazo kabla ya kustaafu?
Cristiano Ronaldo aliangulia kilio baada ya Ureno kufungwa na Ugiriki katika fainali ya Euro 2004
Comments
Post a Comment