Mtandao usiokubali dhambi wavutia wengi
Waanzilishi wa Facegloria wanadai kwamba mtandao huo umewavutia wafuasi takriban laki moja tangu uzinduliwe mwezi Juni.
Kuna maneno
600 yaliopigwa marufuku katika mtandao huo na kuna kibonyezo cha "Amen" kushabikia ujumbe unaobandikwa.
Ummaland, ni mtandao wa kijamii wa kiislamu uliozinduliwa 2013, can una wafuasi 329,000.
Unatoa fursa kwa wanawake kuwa na faragha zaidi na kutoa ujumbe wa nasaha wa kidini kila siku.
Facegloria nchini Brazil kwa sasa unapatikana kwa lugha ya kireno lakini waanzilishi wanataka kuigeuza kwa lugha nyingine pia.
"Kwenye
Facebook unashuhudia uchafu mwingi na ghasia, ndio sababu tulifikiria
kuanzisha mtandao ambao utaturuhusu kuzungumza kuhusu Mungu upendo na
kusambaza neno lake," mtengenezaji mtandao Atilla Barros ameiambia AFP.
Pia ni marufuku kubandika chochote kinachohusiana na mapenzi ya jinsia moja.
Barros
na waanzilishi wenzake watatu walikuwa wakihudumu katika ofisi ya Acir
dos Santos, meya wa Ferraz de Vasconcelos, walipo ubuni mtandao huo wa
kijamii.
Mpaka sasa dos Santos amewekeza $16,000 katika uanzilishi wa mtandao huo
Comments
Post a Comment