MUSEVENI NA MPINZANI WAKE DK, KIZZA BESIGYE WAKUTANA USO KWA USO
Kampala. Wapinzani wawili wa
kisiasa, Rais Yoweri Museveni na mpinzani wake mkuu, Dk Kizza Besigye
wamekutana ana kwa ana kwenye sherehe za Uhuru huko Rukungiri, siku moja
baada ya Rais Museveni kumrushia vijembe Besigye.
Wawili hao wanakutana baada ya Museveni kumtaka
Besigye na Meya wa Jiji la Kampala, Erias Lukwago kuacha kuchochea
machafuko kwenye mji huo kwa nia ya kutaka kuiingiza nchi hiyo kwenye
vurugu kama ilivyo Misri kwa sasa.
Pia aliwataka kuacha kuingia katika mapambano
ambayo hayana faida kwao kwa kuwa mara zote wamekuwa wakishindwa hivyo
ni vyema wakirejea kwenye chama tawala, ambako watapokelewa kwa heshima.
Maoni hayo yaliibua mvutano wa maeneo kutoka kwa
Dk Besigye ambaye amewahi kuwa daktari wa Museveni ambapo alikaririwa na
gazeti la Daily Monitor akihoji “Niombe samahani kwa lipi? Yeye
amejifanya kuwa jaji na hilo ndilo tunapambania,” alisema.
Katika maadhimisho ya leo, dhima kuu ni
‘Kuimarisha fursa za uwekezaji’ ambapo Rais Museveni ndiye mgeni rasmi
na Dk Besigye akihudhuria kwa mwaliko rasmi wa Ikulu.
Comments
Post a Comment