NAPE NAUYO ASEMA HAKUNA NAFASI YA KUKATA RUFAA JINA LIKIKATWA
Dodoma.Chama cha Mapinduzi
(CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa
chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika
nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi
wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa
wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.
Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.
Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa
kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa
kutosha kufanya hivyo.
“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni
haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa
sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.
Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa
chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea
urais kupitia chama hicho.
Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha
Comments
Post a Comment