OKWI AUZWA DENMARK KUANZA KAZI WIKI IJAYO
Okwi
anakwenda kucheza soka katika kikosi cha
Sonderjyske inayoshiriki Ligi Daraja la
Kwanza.
Rais huyo wa Uganda anatarajia kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Denmark kuanza kazi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kila kitu
kimekamilika kuhusiana na Okwi.
“Kweli
Okwi anakwenda Denmark, hii ilikuwa ni sehemu ya makubaliano kati yetu na yeye.
“Kwamba
kama atapata timu nje, basi tumuachie aende.
“Wale
jamaa pia wakatoa ofa nzuri, hivyo hatukuwa na ujanja zaidi ya kumuachia aende
zake,” alisema Hans Poppe, hata hivyo alikataa kuweka wazi kiasi cha fedha
ambacho wamemuuza.
“Hiyo inabaki kuwa siri ya Simba, maana tukitaja basi hesabu zinakuwa nyingi sana
Comments
Post a Comment