RAIS KIKWETE KUVUNJA BUNGE LA 10
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa kuvunja Bunge la 10, mkutano wa 20 wa nchi hiyo.
Hata
hivyo mwandishi wa BBC aliyepo Dodoma, Sammy Awami anaarifu kwamba
wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kinachojumisha baadhi wa
wabunge wa upinzani, wamesema hawatahudhuria ufungaji huo.
Mwaka 2010 wakati Rais Kikwete anafungua Bunge hili wabunge wa upinzani walisusia uzinduzi huo pia.
Wabunge
hawa walitangaza kususia Bunge hili kutokana na uamuzi wa serikali
kuwasilisha miswaada mitatu ya mafuta na gesi kwa hati ya dharura
Pamoja
na mambo mengine, Bunge hili litakumbukwa kwa mjadala mkali uliohusu
maamuzi ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya TSH Bilioni 200 za akaunti ya
Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania
Sakata hili liliwaondoa Mawaziri wawili na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine wa Ikulu na Serikali
Comments
Post a Comment