SIMBA YASEMA MLITHI WA OKWI ANATOKA BRAZIL
Simba
iko katika hatua za mwisho za kumalizana na mshambuliaji raia wa Brazil ambaye
atafanya kazi ya upachikaji mabao kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Okwi ambaye
imemuuza nchini Denmark.
Simba
imemuuza Okwi katika klabu ya Sonderjyske
ya nchini Denmark.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe amesema raia huyo wa Brazil aliwahi kucheza soka katika Falme za
Kiarabu (UAE) na kuwa mmoja wa washambuliaji nyota.
“Tunajua Okwi anaondoka, hivyo ilikuwa ni lazima
kusaka wachezaji wenye uwezo wa juu zaidi ili kuboresha safu yetu ya
ushambuliaji.
"Kuna Mavugo kutoka Burundi, halafu Mbrazili anayekuja hivi karibuni.
“Huyo Mbrazil ni mmoja wa washambuliaji bora kabisa, tuko katika hatua za mwisho naye atakuja mara moja kuanza kazi,” alisema Hans Poppe ambaye ni jembe la usajili Simba
Comments
Post a Comment