TIMU YA NGASSA YATWAA UBIGWA


Free State wakisherehekea ushindi wao wa SAB U21 ya Afrika Kusini
TIMU ya Free State Stars ya Bethlehem, imetwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 21 Afrika Kusini, maarufu kama SAB U21Championship baada ya kuifunga Mpulamanga kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 1-1.
Michuano hiyo ya saba ya U21 inayoandaliwa na Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Afrika Kusini (SAB), ilifanyika Uwanja wa Giant mjini Soshanguve. Na Free State ambayo imemsajili Mrisho Ngassa wa Tanzania Mei mwaka huu kwa ajili ya kikosi cha kwanza, imeweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kutetea taji hilo. Haukuwa ushindi mwepesi kwa Free State kwani walilazimika kuifunga timu ambayo imetoa mfungaji bora wa mashinfdano na mchezaji borsa, Siphamandla Dhlamini. Wasaka vipaji kadhaa walimiminika kwenye michuano hiyo ambayo imekuwa ikizalisha  nyota kibao wa taifa hilo kusaka vipaji vya kupandisha Ligi Kuu.
SAFARI YA FREE STATE HADI UBINGWA SAB U21 2015  Mpumalanga 1. Free State 2 – 1 Mpumalanga 2. Mpumalanga 2 – 1 Western Cape 3. Mpumalanga 4 - 1 Gauteng 4. Mpumalanga 4 – 1 Northern Cape Free State 1. Free State 2 – 1 Mpumalanga 2. Gauteng 2 – 3 Free State 3. Free State 2 – 3 Northern Cape 4. Free State 3 – 0 Western Cape Nusu Fainali Mpumalanga 4 – 2 University Sport SA Limpopo 0 – 2 Free States Fainali: Mpumalanga (1) 1 – 1 (3) Free State
WASHINDI WA TUZO ZA SAB U21 Mwamuzi Bora Msaidizi: Bafana Magagula Refa Bora: Khotso Johanne Kocha Bora: Litheko Marago Mfungaji Bora: Siphamandla Dhlamini Kipa Bora: Kwanele Bidi Mchezaji Bora:  Siphamandla Dhlamini

Comments