UFARANSA KUCHUNGUZA MABAKI YA NDEGE
Mtu anayedaiwa kubaini ushahidi wa kwanza wa mabaki ya Ndege ya Malysia iliyopotea ameelezea mazingira ya yalipopatikana mabaki hayo,na kwamba yeye alikuwa katika shughuli zake za kawaida katika hoteli moja kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.,Ni takribani miezi sita hadi sasa tangu kupotea kwa ndege hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za uhakika kuhusu chanzo cha ajali hiyo
Mabaki hayo yaliyopatikana yanapelekwa Ufaransa kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama ndege ya Malaysia iliyopotea Boing 777,MH 370 iliyokuwa ikitoka Quala lumpa Malaysia ikielekea Beiging China Machi mwaka jana.
John Begue ni mfanyakazi wa fukwe za Saint Andre na ndiye aliyeona mabaki hayo kwa mara ya kwanza,akihojiwa na vyombo vya habari anasema aliona kitu kama mzigo "siku ya Jumanne asubuhi wakati nafanya kazi katika eneo langu nikiwa natafuta mawe kwa ajili ya shughuli zangu ndipo nilipoona kipande cheupe kinachofanana na mabaki ya ndege ambacho nusu yake ilikua ndani ya maji na nusu yake kwenye mchanga.Kukiwa na hali ya upepo baharini ,niliwaita wafanyakazi wenzangu kunisaidia kukibeba kipande hicho na ndipo nilipoona pia sanduku lakini sikulitilia maaanani bali akili yangu ikawa zaidi kuchunguza kipande cha ndege nilichokiona ni muhimu kwangu''
Ndege hiyo ya Malaysia ambayo ilipotea miezi sita iliyopita ilikuwa imebeba abiria 239,ushahidi huu wa mabaki huenda ukawa wa kwanza kufuatilia jitihada za muda mrefu kujua undani wa ajali hiyo
Comments
Post a Comment