VAN PERSIE KUELEKEA FENERBAHNCE YA UTURUKI

Klabu ya Uturuki Fenerbahce ina matumaini ya kuafikia mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie baada ya mazungumzo zaidi.

Awali kilabu hiyo ilikuwa imetoa pauni milioni 4.7 kwa mchezaji huyo wa miaka 31 ambaye alikuwa amepewa kandarasi ya miaka mitatu akiwa na chaguo la kuongezewa mwaka mmoja.
Manchester United inamthamini Van Persie ambaye amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake katika uwanja wa Old Trafford kwa kitita cha pauni milioni 10.
Klabu hiyo ilisisitiza kuwa hakuna maafikiano yalioafikiwa wikendi iliopita lakini mchezaji huyo wa Uholanzi anaaminika kutaka kujiunga na klabu hiyo badala ya kuorodheshwa katika wachezaji wa akiba msimu ujao.

Comments