WATU 25 WAUWAWA MAENEO YA ZARIA NCHIN NIGERIA
Maafisa wa serikali Kaskazini mwa
Nigeria wamesema kuwa watu 25 wameuawa katika shambulio la bomu la
kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.
Ripoti zinasema kuwa watu wengine 32 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
Wengi waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika
kipindi cha majuma 2 yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika
mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa
Boko Haram.
Gavan wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa
waangalifu sana na kuepuka maeneo yaliyojaa watu kwani hayo ndio
yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga.
Gavana Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Inspekta
wa polisi wa Nigeria ameomba wanigeria kuwa makini na waangalifu
akisema kuwa ''kwa sasa inaonekana mabomu yameundwa mengi na kwa hakika
likishaundwa bomu ni vigumu sana kuzuia mashambulizi ya kujilipua kwenye
umati wa watu ilikuzidisha maafa''.
Tayari hofu imetanda katika mji wa Abuja ambapo Polisi wamepiga marufuku uuzaji na uchuuzi katika barabara za katikati ya mji.
Comments
Post a Comment