WATU ZAIDI YA 44 WAUWAWA KATIKA MILIPUKO HUKO NIGERIA

 
Milipuko hiyo imetokea jioni baada ya waislamu kufungua saumu baada ya kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waumini wa kiislamu walikuwa wamekusanyika msikitini kusikiza hotuba ya kiongozi wa kiislamu anayeogopewa.
Punde tu wanaume waliojihami kwa bunduki waliwasili na kuanza kufyetua risasi kiholela kutoka lango kuu la msikiti huo.
Mlipuko ulirushwa miongoni mwa waumini na kuwaua watu hao.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema wapiganaji wa Boko Haram wanaonekana kumlenga kiongozi huyo ambaye katika siku za nyuma ameshutumu mashambulio na harakati za kundi la wanaamgambo hao.
null
Rais Muhammadu Buhari ametaka kikosi cha pamoja kitumwe haraka
Mlipuko mwingine uliotokea karibu na chuo kikuu uliwalenga watu waliokuwa wakifungua saumu baada ya kufunga.
Polisi katika mji wa Jos hawakuweza kutoa taarifa zaidi, lakini wakaazi wanasema idadi ya waliofariki ipo juu.
Watu watano wameuawa katika mlipuko mwingine wa kujitoa muhanga uliotokea mapema asubuhi kwenye kanisa mjini Potiskum kaskazini mashriki mwa Nigeria.
Milipuko ya Jumapili yamejiri baada ya wiki nzima ya ghasia zilizosababisha vifo vya watu takriban mia mbili.
Serikali imeshutumu mauaji hayo ambayo katika mwezi uliopita yameongezeka.

Comments