ALIEUA TEMBO 114 APEWA DHAMANA KENYA

 
Feisal amekanusha mashtaka yote dhidi yake.
Mahakama kuu ya Kenya imemuachilia kwa dhamana mshukiwa mkuu wa uwindaji haramu aliyekamatwa nchini Tanzania.

Feisal Mohammed Ali,aliyeorodheshwa katika nafasi ya sita ya watuhumiwa wa uwindaji haramu na biashara ya kuuza pembe za ndovu ameachiliwa kwa dhamana baada ya mawakili wake kuomba mahakama hiyo imruhusu apokee matibabu .
Hata hivyo afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma nchini humo tayari imeonesha kutoridhishwa kwake na uamuzi uliofikiwa na hakimu Davis Karani katika mahakama ya Mombasa.
Hii si mara ya kwanza kwa mahakama za Kenya kumruhusu mshukiwa huyo kuondoka.
Mwezi Machi,Feisal alipewa dhamana na mahakama ya Mombasa lakini afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma ikakata rufaa iliyokubaliwa na mahakama ya juu.
 
'Aliyeua' tembo 114 apewa dhamana Kenya
Hapo jana hakimu Karani alimpa Feisal dhamana ya shilingi millioni kumi za Kenya sawa na dola laki moja $100,000 za mMarekani
Feisal anakabiliwa na shtaka la usafirishaji kinyume cha sheria kwa tani mbili za pembe za ndovu yenye thamani ya dola milioni $4.5 za Marekani, umiliki wa pembe za ndovu kinyume cha sheria.
Yamkini Feisal anatuhumiwa kuwa mmiliki wa pembe za ndovu 114.
Upande wa mashtaka unadai kuwa yeye ndiye kiunganishi kati ya wawindaji haramu wanaolaumiwa kwa kuuwa tembo 33,000 kati ya mwaka wa 2010-2012 barani Afrika.
 
Feisal anatuhumiwa kuwa mmiliki wa pembe za ndovu 114.
Feisal amekanusha mashtaka yote dhidi yake.
Kasha la pembe hizo za ndovu zilikuwa zimefichwa katika bohari moja ya wauzaji magari mjini Mombasa.
Punde baada ya polisi kuvamia eneo hilo Feisal alitorokea Tanzania alikokamatwa na polisi wa huko baada ya ombi kutolewa kupitia mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol

Comments