Bolt atawala mita 100 Beijing


 
Image caption Usain Bolt
Bingwa wa dunia was mbio za matimko za mita 100 kwa upande wa wanaume,Usain Bolt wa Jamaica, amejifurukuta na kuwapiku wapinzani wake wakuu alipohifadhi taji lake la dunia mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kushuhudia fainali hiyo katika uwanja wa kimataifa Birds Nest Beijing China.

Bolt alitoka nyuma na kuukata utepe katika fainali iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na ghamu na watu wengi zaidi katika mashindano ya riadha duniani yanayoendelea nchini China.
 
Image copyright no credit
Image caption Bolt atawala mita 100 huko Beijing
Licha ya kupigiwa upatu kuwa mashindano magumu kwa kujumuisha majina yote tajika yakiwemo wanaridha wakuu wa mbio hizo, Asafa Powell, Mmarekani Tyson Gay na Justin Gatlin,ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa kupatikana na hatia ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu,Bolt alikata utepe wa kwanza.
 
Image copyright AP
Image caption Gatlin alimaliza chini ya nukta moja nyuma ya Bolt
Gatlin alimaliza chini ya nukta moja nyuma ya Bolt aliyeandikisha muda wa sekunde 9.79.
Raia wa Canada, Andre de Grasse na Mmarekani Trayvon Bromell walisajili muda wa sekunde 9.92 na kutuzwa medali ya shaba.
 
Image copyright Getty
Image caption 'Endapo Justin angeibuka mshindi basi ushindi wake ungelitia doa jina la mchezo wa riadha''
Mwandishi wa BBC mjini Beijing John Nene, anasema kuwa Gatlin alikuwa na rekodi ya kushiriki mbio 28 bila ya kushindwa msimu huu na japo alikuwa amepigiwa upatu kuibuka mshindi huko Beijing,Kulikuwa na hofu kubwa yakuwa endapo angeibuka mshindi basi ushindi wake ungelitia doa jina la mchez o wa riadha ambao umekumbwa na madai hivi majuzi ya matumizi makubwa ya madawa za kuongeza nguvu yaliyopigwa marufuku.
Bolt atakumbukwa kwa kuibuka kidedea kati8ka mbio za matimko alipozoa medali za dhahabu katika mbio za mita 100 na mita 200 katika mashindano ya olimpiki mwaka wa 2008 huko huko Beijing.

Comments