DI MARIA RASMI SASA MCHEZAJI WA PSG MPAKA 2019

di maria
Winga hatari wa Argentina aliekuwa anakipa katika klabu ya Man united iliopo nchini wingereza jana tarehe 6/8/2015  majira ya saa 8 mchana kwa saa za Africa mashariki alisaini mkata na kujiunga rasmi na timu yake mpya PSG kwa ada ya paundi mil 44.3 akitokea old trafod ambako iliwagalimu mashetani hao wekundu paundi mil 59 kumtoa winga huyo huko hispania katika jiji la madrid.
Angel Di Maria baada ya kusafiri kwa masaa 20 na kufika Qatar ambapo siku ya Jumanne alifanyiwa vipimo vya afya, hatimaye amefaulu tayari kwa kujiunga na PSG inayoshiriki ligi ya Ufaransa.
Akiongea na BeIN Sports, Di Maria alisema maneno haya, “Nina furaha kwa kujiunga na PSG, ninachokijua ni kwamba PSG iliyoshinda makombe mengi kwenye msimu uliopita kule Ufaransa. Hiki ni kitu muhimu sana kwa club. Napia nataka kuvuka kihunzi ambacho ni robo fainali ya UEFA champions league pamoja na hii club. Naenda kujaribu kujitoa kadri niwezavyo kwenye huduma ya hii timu ili tufanikiwe. Tutajaribu kufika mbali kadri tunavyoweza ili tushinde ubingwa wa Ulaya”.
Di Maria ameweka wazi lengo lake na club hiyo ni kwamba kuchukua kombe la UEFA. Tuendelee kufuatilia mpango mzima utakavyoenda

Comments