DK. CHEGENI AMBWAGA WAZIRI KAMANI KURA ZA MAONI HUKO MKOANI SIMIYU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Raphael Chageni, amembwaga Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk.
Titus Kamani katika kura za maoni za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge
kwenye Jimbo la Busega mkoani Simiyu.
Hatua ya kushindwa kwa Dk. Kamani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa
Mkoa wa Simiyu, imemfanya aungane na mawaziri na manaibu waziri wa
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete walioangukia pua katika mbio za kusaka
kurejea katika majimbo yao.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku kadhaa za vuta nikuvute
zilizosababisha kuibuka kwa vurugu na hata kuporwa kwa nyaraka za
matokeo ya kura hizo.
Akimtangaza Dk. Chegeni kuwa mshindi katika mchakato huo wa kura za
maoni, Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya
Wazazi Wilaya ya Busega, William Bendeke, kwa niaba ya katibu wa wilaya,
alimtangaza mshindi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa, huku pia Mkuu wa
Wilaya hiyo, Paul Mzindakaya akishuhudia utangazaji wa matokeo hayo.
Bendeke alimtangaza Dk. Chegeni mshindi kwa kura 13,048 dhidi ya kura 11,829 alizopata Dk. Kamani.
Akizungumza na wananchi waliofika wakati wa kutangazwa kwa matokeo
hayo, Dk. Chegeni aliutaka uongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu kutenda haki
katika vikao vya uteuzi na kuacha kuminya demokrasia ndani ya chama
Comments
Post a Comment