Hii ya magereza 9 duniani kubadilishwa kuwa mahoteli makubwa imenifikia, Africa ipo moja tu!
Nimekutana na stori moja kwenye mitandao inayohusiana na magereza ya zamani ya wafungwa, yamekusanywa magereza 9
ya sehemu mbali mbali duniani na kubadilishwa kuwa kitu tofauti kabisa,
na ukiyaona hutoamini kuwa majengo hayo yalishawahi kuwa magereza ya wafungwa!
Kwenye yale maeneo ambayo Serikali waliacha kuyatumia kama maeneo ya magereza ya wafungwa yamechukuliwa na kubadilishwa kuwa hoteli au shule mtu wangu, majengo ni yale yale sema ubunifu mdogo tu umetumika kuyageuza majengo hayo kuwa sehemu ya vivutio kwa watalii.
Na kwa msaada
wa teknolojia ya kisasa kabisa sehemu hizi zimegeuzwa kuwa sehemu nzuri
sana, zenye mvuto na kama ukitembelea maeneo hayo bila kujua historia
ya sehemu hiyo itakuwa vigumu sana kwa wewe kujua kuwa jengo au eneo
hilo lilikuwa la wafungwa magereza.
Hapa chini
nimekusogezea picha 9 za maeneo na magereza mbali mbali duniani ambayo
kwa sasa zinaweka headlines tofauti na miongoni mwa picha hizi kuna moja
kutoka Lagos Nigeria iliyoweka headlines.
Comments
Post a Comment