JUSTIN BIEBER AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE
NYOTA
wa muziki wa RnB nchini Marekani, Justin Bieber, amewaomba radhi
mashabiki wake nchini Uingereza baada ya kutangaza kusitisha onyesho
alilotakiwa kulifanya nchini humo.
Msanii
huyo mwenye umri wa miaka 21, alitarajia kufanya onyesho hilo Agosti 28
mwaka huu nchini humo, lakini amesitisha bila kutaja sababu za msingi.
“Naomba
radhi kwa mashabiki wangu nchini Uingereza kwa kusitisha kufanya shoo
Agosti 28, lakini lazima nitaifanya muda mfupi ujao.
“Nimeona
nitumie muda huu kujipanga vizuri ili niweze kuwapa shoo yenye ubora
kutokana na ninavyokubalika na idadi kubwa ya mashabiki, hivyo naomba
uvumilivu wenu,” alieleza Berber.
Comments
Post a Comment