KENYA NA ETHIOPIA ZA SHINDA DHAHABU

 
Rudisha
David Rudisha alikabili maswali mengi kuhusu uwezo wake wa kuimarika katika mbio za mita 800 baada ya kushinda dhahabu katika mashindano ya riadha ya Beijing.

Bingwa huyo wa mbio za Olimpiki na bingwa wa rekodi ya dunia katika mbio hizo ambaye pia alishinda taji la ulimwengu mwaka 2011,aliongoza kutoka mbele na kuweza kuweka mda wa dakika 1sekunde 45.84 mbele ya mwanariadha wa Poland Adam Kszczot.
Amel Tuka wa Bosinia Haerzegovina ambaye anashikilia mda bora mwaka huu alichukua medali ya shaba.
Hatahivyo mbio hizo zilikosa msisimuko wake baada ya mwanariadha wa Botswana Nijel Amos na mwenzake wa Ethiopia Mohammed Aman kushindwa kufuzu katika fainali.
 
Image caption Dibaba
Wakati huohuo Mkenya Nicholas Bett alinyakua medali ya dhahabu baada ya kuweka mda bora wa sekunde 47.79 katika mashindano ya mbio za mita 400 kuruka viunzi.
Raia wa Urusi Denis Kudryavtsev alichukua medali ya fedha huku Jeffery Gibson wa Bahamas akimaliza wa tatu.
Ilikuwa medali ya kwanza ya Kenya katika mbio fupi katika mashindano ya dunia.
Katika upande wa wanawake mwanariadha wa Ethiopia Genzebe Dibaba alichukua dhahabu katika mbio za mita 1500.
 
Image caption Bett
Muingereza Laura Muir alimaliza wa tano katika mbio na Paula Radcliff na kuongezea kuwa raia huyo wa Uskochi anaweza kuondoka Beijing akiwa na furaha.
Faith Chepngetich Kipyegon alichukua nafasi ya pili huku Sifan Hassan wa Uholanzi akimaliza wa tatu

Comments