MABAKI YA WATU 40 YAZIKWA HUKU SOMALIA
Shughuli ya kuzika
mabaki ya zaidi ya watu arobaini imefanyika katika eneo lililojitangazia
uhuru la Somaliland. Mabaki hayo yalipatikana katika kaburi moja
Mifupa hiyo ilipatikana wakati mitaro ya mabomba ya maji ilipokuwa ikichimbwa katika mji mkuu Hargeisa.
Inaaminika watu hao waliuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka elfu moja mia tisa themanini na nane.
Idadi kubwa ya watu hao walikuwa watoto na akina mama.
Waliuawa wakati wa mashambulio ya mabomu yaliyofanyika mjini Hargeisa wakati huo ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilikuwa vikiendelea.
Comments
Post a Comment