MKWASA ATANGAZA KIKOSI KIPYA KWAJILI YA KUIVAA NIGERIA
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi
cha wachezaji 29 watakaongia kambini siku ya Jumapili Agosti 9, katika
hoteli ya Tansoma iliyopoe eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki
moja ya mazoezi.
Katika kikosi hicho
alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano
wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Professionals), ambao baadae
watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba
2015 nchini Uturuki.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka
kambi ya siku kumi jijini Istambul – Uturuki, ambapo itacheza michezo
miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea
nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji watakaongia kambini
Jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam
FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu
Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi wa kati; Hassan Isihaka
(Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji:
Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji
ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji wa pembeni; Orgenes
Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke,
Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku
washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid
Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wa kimataifa
waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini
nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu
(TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) na
Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town –
Uingereza).
Comments
Post a Comment