Museveni amsuta Raila kuhusu Sukari
Museveni amusuta Raila kuhusu Sukari
Rais
wa Uganda Yoweri Museveni amemsuta kiongozi wa upinzani wa Kenya, Raila
Odinga, kwa kupinga mkataba wa uuzaji wa sukari uliotiwa sahihi majuzi.
Museveni alisema kuwa Odinga hafaaamu anachokisema.
''hata ndugu yangu odinga anazungumzia maswala ya sukari,bila kufahamu ukweli wa maswala hayo'' Museveni.
Kenya imekuwa ikizuia sukari yetu na mahindi ilihali Uganda imekuwa ikiagiza bidhaa za thamani kubwa pasi na kujali kuwa inawasaidia kujiendeleza.
''Wewe ni mkurugenzi wa kampuni ilihali kazi yako kubwa ni kuzuia sukari ya Uganda isiingie Kenya.
'Nafikiri nitampigia Raila simu nimwambie kuwa sukari ya Uganda itaingia Kenya sawa na vile mali ya Kenya inaingia Uganda bila vizingiti' aliongezea Museveni.
Rais Museveni aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wageni waalikwa na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki lililoanza vikao vyake jiji Kampala Uganda.
Museveni alisema mataifa wanachama wa muungano wa kanda hii ya Afrika Mashariki na kati sharti yafuate kanuni za muungano ikiwemo Kenya.
Uganda kwa sasa inasaga sukari tani 450,000 huku ikitumia takriban tani 320,000 na hivyo inasalia takriban tani 145,000 za sukari.
Hii ndiyo sukari ambayo sasa itaruhusiwa kuuzwa nchini Kenya.
Kwa Upande wake Kenya inazalisha takriban tani 600,000 ya sukari huku ikihitaji kati ya tani 800,000 na 850,000 kwa hivyo inanakisi ya takriban tani 250,000 za sukari kukidhi mahitaji ya raia wake.
Wazo hilo limepuziliwa mbali na serikali ya Kenya ambayo imekuwa ikisisitiza kuwa sukari ya Uganda itaendelea kuingia Kenya chini ya mpango wa jumuia ya Afrika Mashariki COMESA.
Comments
Post a Comment