NAIBU KATIBU MKUU WA CUF ASEMA "ASKALI AKIFA MAPAMBANO YANAENDELEA"

Mtatiro
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Julius Mtatiro, amesema kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ni sawa ana askari kufia mstari wa mbele na mapambano yanaendelea kama kawaida.

Mtatiro alitoa kauli hiyo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook mjini Dar es Salaam jana.
“Mapambano yaendee, askari amekufa akiwa  mstari wa mbele wakati vita inakaribia kuisha, ni bahati mbaya, chukueni mwili wake, upeni heshima zote za mwisho kisha uhifadhini na kukumbuka mchango wa askari huyo.
“Si muda wa kumbeza na kumsimanga, si muda wa kumuombea mabaya.
“Wanaweza kufa askari wengi dakika za mwisho za mapigano, lakini kusaka ushindi vitani ni jukumu la askari waliobakia…hata wakibaki wachache ni lazima washikamane na vita iendelee.
“Huu siyo wakati wa kujiuliza kama sababu za kuingia vitani zilikuwa sahihi au la, huu siyo muda wa kuacha vita na kuanza mjadala juu ya askari shupavu aliyeuawa mstari wa mbele, huu ni muda wa kupigana vita… vitani hakuna msalie mtume na ukitaka salamu ya upande wa adui umekaribisha kifo chako. Vita haina macho, yeyote yule anaweza kuuawa,”ilisema taarifa hiyo.

Comments