Pedro:Nilikataa ombi la timu za Manchester
Mchezaji mpya wa
Chelsea Pedro amefichua kwamba alikataa kujiunga na timu zote mbili za
Manchester na badala yake kujiunga na Chelsea.
Winga huyo alifurahishwa na wazo la yeye kuhamia London baada ya kuamua kwamba angesalia Barcelona ili kuonekana katika picha.
Amesema kuwa alikataa ombi la kujiunga na timu hizo za Manchester huku akisema kuwa ushirikiano wa Jose Mourinho,Cess Fabregas na makao ya Stamford bridge ni baadhi ya vivutio vilivyomvutia.
Kilabu ya Manchester United ilikuwa kifua mbele katika kutafuta saini ya Pedro lakini ni Chelsea ilioharakisha uhamisho huo huku Mourinho na Fabregas wakihusika pakubwa katika kumrai ,mchezaji huyo.
Comments
Post a Comment