POLISI YAKAMATA BUNDUKI 16 ZILIZO POLWA KITUO CHA STAKISHARI
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limesema limeshakamata bunduki 16 kati ya 21 zilizoporwa kwenye Kituo cha Stakishari.
Bunduki
hizo ziliporwa Julai 12 wakati watu wanaoaminika kuwa ni majambazi
walipovamia kituo hicho cha polisi, Ukonga – Dar es Salaam na kuua
askari wanne na watu wengine watatu.
Jana, Naibu
Kamishna wa Kanda ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia
waandishi wa habari kuwa zaidi ya majambazi 10 wameshakamatwa na polisi
wanaendelea kuwahoji kuhusu tukio hilo.
“Silaha
zilizokuwa zimebaki ni tano, 16 zimeshakamatwa na hizo tano ndizo
tunafanya bidii ya kuzipata. Niwahakikishieni kuwa zitapatikana,”
alisema Sirro.
Alisema watuhumiwa waliovamia kituo hicho walikuwa zaidi ya 15 na walitumia mbinu mpya ambayo Polisi hawakuitegemea.
Wakati
huohuo; Jeshi la Polisi limewakamata watu watatu kwa tuhuma za mauaji
ya ofisa wa Polisi, Elibariki Palangyo yaliyotokea nyumbani kwake Yombo
Kilakala, usiku wa Agosti.
Katika tukio jingine, polisi
inawashikilia watu wanne wakituhumiwa kukutwa na vipande vinne vya meno
ya tembo vyenye thamani ya Sh30 milioni juzi, saa 1.30 usiku huko
Tandale kwa Mtogole.
Comments
Post a Comment