SAFU YA USHAMBULIAJI YAENDELEA KUWA KIKWAZO CHA USHINDI UNITED

 
Newcastle United ilijitahidi nakuwadhibiti wenyeji wao Manchester United katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza iliyomalizika muda mchache uliopita uwanjani Old Trafford.

Newcastle ilijifurukuta na kuvunja rekodi ya kushinda mechi zote msimu huu iliyokuwa imewekwa na Man united.
Chini ya mkufunzi Steve MClaren, Newcastle United ilikaza buti na kuwanyima washambuliaji wa manchester fursa ya kushambulia lango lao.
Aidha vijana hao wa Mclaren walijizolea alama yao ya pili msimu huu.
Vijana wa kocha Louis van Gaal hata hivyo walitamaushwa na kauli ya refarii aliyepuliza kipenga na kuashiria bao la mshambulizi Wayne Rooney kuwa halikufaa na kuwa alikuwa ameotea
Nusura Newcastle wafunge bao la kwanza kupitia mkwaju wa Aleksander Mitrovic uliogonga mwamba wa lango baada ya kuwapita walinzi na kipa wa manchester.
Mshambulizi huyo wa Serbia aliwaacha walinzi wa manchester hoi.
Muda mchache baadaye nipe nikupe kati ya washambulizi wa Manchester nusura izae matunda isipokuwa tu juhudi za Tim Krul wa Newcastle aliyezima kombora la Javier Hernandez.
 
Sare tasa Old Trafford; Man Utd 0 - 0 Newcastle
Mashambulizi hayakuishia hapo, vijana wa van Gaal waliendelea kushambulia lango la Newcastle hadi dakika ya mwisho dakika tano za ziada Chris Smalling alipogonga mchuma wa
Newcastle sekunde chache tu kabla ya mechi hiyo kumalizika.
Man Utd 0 - 0 Newcastle
Pamoja na timu ya mashetani wekundu kufanya usajili mzuri sana msimu huu lakin mpaka sasa bado safu ya ushambuliaji inayo ongozwa na rooney imeonekana kutopata mabao kama ambavyo ilitalajiwa 

Hata ivyo kwa upande wa kocha Mholanzi wa man united alikitetea kikosi chake na kusema walicheza vizuri sema matatizo madogo madogo ambavyo yeye pamoja na benzi nzima la ufundi wameyaona watayafanyia kazi ili waweze pata ushindi kwa mechi zinazofuata

Comments