SIMBA YAACHANA NA MAVUGO SASA YAGEUKIA KWA NIMUBONA KUWASILI LEO DAR TAYARI KWA KUJIUNGA NA SIMBA HUKO ZENJI

Image result for SIMBA SC

SIMBA SC imeamua kuachana na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo baada ya klabu mbili za nchini humo kuopandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 zilizokubakiwa awali.

Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva ameviambia  vyombo vya habari  leo kwamba, pamoja na jitihada za kutuma biongozi Bujumbura kwa mijadala mirefu suala hilo limeshindikana na sasa wanaelekeza nguvu zao katika kusaka mchezaji mwingine.  “Wakati mchakato huu ukiendelea Simba SC ilikuwa inaendelea na mazungumzo na washambuliaji kadhaa wa kimataifa Ili kuwa na wigo mpana wa kuchagua. Tunaamini tutasajili mchezaji mzuri na bora ambaye thamani na uwezo wake utashabihiana au kuwa zaidi,”amesema Aveva. Aveva amesema walikubaliana mchezaji asajiliwe kwa Sh 110 milioni baada ya michuano ya Ligi Kuu na Kombe la FA Burundi na Simba SC ilimtuma Makamu wake wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aende Bujumbura kukamilisha majadiliano na uongozi wa Vital’O juu ya usajili wa Laudit Mavugo.  Lakini ajabu, Vital’O wakabadilika na kuongeza maradufu thamani ya mchezaji huyo pamoja na vipengele vipya vya mauzo kinyume na makubaliano ya awali. “Thamani mpya ya mchezaji imepandishwa na kuwa Tshs 200 milioni kutoka ile ya awali ya Tsh 110 milioni ambazo zilijumuisha gharama za kumlipa mchezaji.”amesema Aveva. Aidha, kumeibuka pia mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo, hivyo nayo kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo. “Licha ya mkanganyiko wa umiliki wake, Vital’O imedai kuwepo kipengele kipya kinachodai mapato ya asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Simba SC kwenda klabu nyingine,”amesema. Lakini pamoja na hayo, Aveva amesema Simba SC imefarijika kwa kumpata beki wa kimataifa wa Burundi kutoka klabu ya Vital’O, Emery Nimubona ambaye atawasili nchini leo na moja kwa moja kwenda kujiunga na timu kambini Zanzibar. Beki huyo wa zamani wa Athletico Olympic ya Burundi pia, anacheza beki zote mbili, kulia na kushoto.

Comments