TOP 10 YA WACHEZAJI WALIOSAJILIWA KWA ADA KUBWA
Kila mwishoni mwa msimu wa Ligi mbalimbali duniani vilabu husika huwa na utamaduni wa kuanza kufuatilia wachezaji sahii watakao ongeza nguvu katika vilabu vyao na namna ambavyo watawapata. Siku hizi kila klabu inapomuhitaji mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine uhamisho wake uhitaji ada kubwa kutokana na kiwango cha mchezaji husika.
Klabu mbalimbali duniani imekuwa kawaida sana kukuta wakinunua mchezaji kwa gharama ya juu, Real Madrid
wao huwa hawajali gharama ya mchezaji bali huwa wanaangalia ni kweli
wanamuhitaji na anauwezo wa kusaidia timu yao basi hawaoni ugumu kuingia
mfukoni na kutoa mamilioni ya pound ili tu kuhakikisha wanampata
mchezaji wamtakaye na kuboresha kikosi chao.
Nimeona nikusogezee mtu wangu wa nguvu Top 10 ya wachezaji walio katika rekodi ya gharama ya usajili kwa muda wote.
10. Radamel Falcao pamoja na klabu nyingi kuwa zinamuwania wakati huo akiwa katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, pound milioni 51 zilitosha kwa klabu ya Monaco kuipiku klabu ya Chelsea na zingine zilizokuwa zinamuwania mshambuliaji huyo wa Colombia na kufanikisha kumpleleka Ufaransa. Falcao kwa sasa anaichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza kwa mkopo.
9. Ni Edinson Cavani mshambuliaji wa kimataifa kutokea Uruguay ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa uhamisho wake wa Pound milioni 55 kutoka katika Klabu ya Napoli ya Italia kwenda PSG upo katika hi rekodi.
8. Ricardo Kaka uhamisho wake wa pound milioni 56 kutoka katika klabu ya AC Milan kwenda katika klabu ya Real Madrid ya Hispania uliingia katika rekodi ya klabu hiyo na hata kwa wachezaji wengine waliowahi kusajiliwa kwa dau kubwa. Kaka kwa sasa anaichezea klabu ya Orlando City.
7. Zlatan Ibrahimovic
mwaka 2009 alikuwa ni headlines katika kila chombo cha habari
kinachojiuhusisha na utoaji wa habari za michezo, baada ya kusajiliwa
kwa dau la pound milioni 59 kutoka katika klabu ya Inter Milan na kujiunga na FC Barcelona ya Hispania, Zlatan kwa sasa anaichezea klabu ya PSG.
6. Angel Di Maria uhamisho wake wa pound milioni 59.7 kutoka Real Madrid kwenda katika klabu ya Man United ya Uingereza haukuwa ni rekodi katika klabu ya Man United pekee ila umeingia katika list ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi. Di Maria kwa sasa yupo katika klabu ya PSG aliyojiunga nayo msimu huu.
5. James Rodriguez mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, michuano ya Kombe la dunia 2014 iliyofanyika Brazil ili ongeza thamani yake kwani ni moja kati ya wachezaji waliyocheza kwa kiwango cha juu hivyo Real Madrid hawakuona ugumu kutoa pound milioni 63 na kuilipa Monaco kwa ajili ya staa huyo.
4.Vilabu vingi viliwania saini ya Neymar bila mafanikio ila klabu ya FC Barcelona inayosifika kwa kuibua vipaji ilikubali kulipa pound milioni 71.5 na kumsajili nyota huyo kutoka katika klabu ya Santos ya Brazil.
3.Mwaka 2014 ndio mwaka ambao klabu ya FC Barcelona ilifanikiwa kumnasa nyota wa Liverpool wakati huo Luis Suarez kwa dau la pound milioni 75 na kumfanya staa huyo kutua Nou Camp.
2. Uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Man United kwenda Real Madrid uliingia katika headlines kwani ulikuwa wa dau kubwa na ukilinganisha na jina lake Ronaldo. hivyo pound milioni 80 zilitosha Man United kushawishika kumuuza staa huyo.
Gareth Bale alikuwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza ni mmoja kati ya wachezaji wenye kasi zaidi hivyo umahiri wake uwanjani uliwafanya Real Madrid ya Hispania kutoa pound milioni 86 na kuilipa Spurs ili wapate baraka za kumnasa nyota huyo.
Comments
Post a Comment