TUNDU LISSU AFUNGUKA KUHUSU PROFESA LIPUMBA
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema hatua ya Profesa Lipumba kujiuzulu ni sawa na jenerali wa jeshi aliyeanguka katikati ya mapambano ya kuelekea Ikulu na harakati za mageuzi na mabadiliko alizoanza miaka 20 iliyopita.
Akizungumza
nje ya Hoteli ya Ledger Bahari Beach kilipofanyika kikao cha Kamati Kuu
ya Chadema jana, Lissu alisema katika mapambano kuna majenarali na
askari wa kawaida, lakini Profesa Lipumba ni sawa na jenerali
aliyeanguka katikati ya uwanja wa mapambano ya mabadiliko.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Halima Mdee alisema
Profesa Lipumba alikuwa kikwazo katika maamuzi ya Ukawa.
“Sishangai
kwa sababu tulikuwa tunajua kuwa yeye ndiyo kikwazo cha Ukawa tangu
mwanzo wa vikao vyetu. Alikuwa na sababu nyingi, akimaliza hii anaibua
nyingine,” alisema Mdee.
Mbunge wa Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa alimfananisha Profesa Lipumba na abiria wa treni
anayeamua kushukia njiani kabla hajafika anakokwenda.
Comments
Post a Comment