Wahamiaji 3000 mashakani Mediterranea
Walinzi
wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa wanaongoza shughuli za kuwaokoa
wahamiaji kama elfu-tatu hivi ambao wametuma ishara ya kuwa taabani
kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika
uokozi.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.
Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia .
Jarida moja la Norway Aftenposten, limesema kuwa manuari ya kijeshi ya taifa hilo Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko mashakani.
Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema leo kabla ya kurejeshwa tena huko huko kushiriki operesheni hii ya kuoko nafsi za watu wanaokisiwa kuwa takriban 3,000
Comments
Post a Comment