WANASAYANSI WASEMA KUWA UMME WENYE UMBO DOGO NA MFUPI NI TATIZO
Wanasayansi
wengi wa tiba wametoa machapisho mengi ya kitafiti kuhusu urefu na
upana wa uume nia na madhumuni ni kujibu swali juu ya wastani wa uume
kwa wanaume wengi duniani ni upi.
Baadhi ya wanaume
wamekuwa wakiishi kwa hofu na kukosa kujiamini katika uhusiano wao
wakihisi kuwa wana uume ambao ni mdogo usioweza kumridhisha mwenza wa
kike.
Hofu hiyo inawezekana ni kutokuwa na ufahamu
sahihi juu ya maumbile yao yalivyo, wengi wanakosa taarifa sahihi kutoka
wataalamu wa afya wenye uelewa wa jambo hili.
Hofu ya
wanaume inaongezeka kila siku hasa kutokana na utitiri wa matangazo ya
magazeti, mitandaoni, hadithi za vijiweni na matangazo ya waganga wa
kienyeji mitaani wanaojitangaza kuwa na dawa na vifaa tiba vya kuongeza
urefu na upana wa uume.
Dondoo zifuatazo zinajumuisha
ripoti mbalimbali za kitafiti, ikiwamo yale yaliyochapishwa katika
majarida makubwa na maarufu duniani ikiwamo ya Science today, Men’s
health na British Journal of Urology international.
Asilimia
85 ya wanawake wanaridhika na urefu na upana wa maumbile ya uume wa
wenza wao, ingawa wanaume wenyewe hawana uhakika wa jambo hilo, huku
asilimia 45 ya wanaume wakiamini kuwa wana maumbile madogo.
Tafiti
mbalimbali zilikuja na hitimisho kuwa wastani wa urefu wa uume ukiwa
haujasimama, ukiwa katika hali ya ulaini ni kati ya sentimita 7 hadi 10
au inchi 2.8 hadi 3.9, urefu unapimwa kuanzia katika shina la uume mpaka
katika kichwa.
Wakati kipimo cha mzunguko wa uume ukiwa haujasimama ni kati ya sentimita 9 hadi 10 au 3.5 hadi 3.9
Urefu
wa uume unapokuwa umesimama ni kati ya sentimita 12 hadi 16 au inchi
4.7 hadi 6.3. Urefu wa mzunguko wa uume ukiwa umesimama ni kati ya
sentimita 12 au inchi 4.7.
Dondoo nyingine ya tafiti
inaonyesha kuwa wanaume wenye unene uliopitiliza na wenye umri mkubwa
wengi wao wana “urefu mfupi” wa uume ukiwa umesimama.
Maumbile
ya uume yanatofautiana kati ya jamii moja na nyingine, bara moja na
jingine. Wanaume wanaotokea Asia wana maumbile madogo ya uume
ukilinganisha na wanaume wa bara la Afrika.
Wanawake
wengi huwa hawajali urefu na upana wa uume wa wenza wao, pengine ni
kutokana na ukweli kuwa kufika kilele cha tendo kwa wanaweka si lazima
kumuingilia, wanaweza kufika kileleni hata kwa njia nyingine hata kwa
kutomaswa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama
Ernst Grafenberg mwenye asili ya Ujerumani, ndiye mgunduzi wa sehemu ya
kike ambayo ndio inaelezwa ina msisimko wa kipekee kuliko nyingine
yoyote katika sehemu za kike.
Sehemu hiyo ijulikanayo kama G-spot ambayo ipo sentimeta 5.1-7.9 au nchi 2-3 tu kuanzia nje ya uke kuingia ndani.
Inaelezwa
kuwa unaweza kuwa na uume mdogo lakini ukamridhisha mwenza wako na
kumfikisha kileleni kutokana na sehemu hiyo huweza kusisimuliwa hata na
uume mdogo.
Comments
Post a Comment