WATOTO 10 WAUAWA KATIKA MLIPUKO AFGANISTAN
Mlipuko mkubwa nje
ya kituo cha kusambaza gesi katika mji wa Herat nchini Afghanistan,
umesababisha vifo vya watoto kumi na mtu mzima mmoja.
Msemaji wa hospitali amesema kwamba watu wengine 18 wamejeruhiwa katika eneo hilo ambalo hutumika kama kambi ya wakimbizi.
Picha katika mitandao ya kijamii inaonyesha miale ya moto juu angani.
Haijabainika iwapo mlipuko huo ulikuwa ajali , au shambulio
Comments
Post a Comment