ABUBAKARY ZUBEIRY ACHAGULIWA RASMI KUWA MUFTI MKUU WA TANZANIA
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) jana limemchagua Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Africa Dream mjini
Dodoma, Tume ya Dini ya Kiislamu imemchagua Sheikh Zubeiry kwa kura 310
za ndiyo baada ya kuingia kwenye uchaguzi huo akiwa mgombea pekee.
Akitangaza
matokeo hayo, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Alhaji
Habib Ndassiwa alisema majina mawili yaliyotoka kwenye Baraza la Ulamaa
yalikuwa ni ya Sheikh Ally Muhidini Mkoyogole na Sheikh Zubeiry.
Hata hivyo Sheikh Mkoyogole alijitoa na hivyo kumuacha Sheikh Zebeiry kuwa mgombea pekee.
Mufti
Zubeiry aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya juu katika dini ya Kiislamu
mnamo Juni 22 mwaka huu baada ya kifo cha Mufti Issa Shaaban Simba
kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa
amelazwa kwa matibabu.
Alitakiwa
kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (Siku Tisini) hadi
Septemba mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi
hiyo.
Comments
Post a Comment