BABA MZAZI WA DEPAY AMPIGIA MAGOTI MWANAE
Baba
mzazi wa mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi,
Memphis Depay ajulikanaye kama Denis amesema yuko tayari kurudisha
mahusiano na mwanae huyo kwani ana mkumbuka sana.
Depay ambaye alikataa kutumia
jina la baba yake, Denis na badala yake akaamua kutumia jina la Memphis
walitengana na baba yake mzazi tangu akiwa na miaka 4 tu kitu
kilichopelekea waondoke na mama yake hadi Uholanzi ambako wanaishi hadi
leo.
Denis (mzazi wa Depay) ni raia wa
Ghana na sasa anajutia kutokuwa na mahusiano na mwanae kwa kipindi cha
miaka 17 hivi sasa. Mzee huyo anasema anamkumbuka sana mtoto wake na
anamuomba wamalize tofauti zao ili warudi kuwa kitu kimoja.
Mzee huyo mwenye miaka 50 anasema
kimsingi hakumkataa mtoto wake, na kwamba aliumia sana kumuona mwanae
akiongea katika YouTube kusema hakutaka kulitumia jina halali la baba
yake, kitu kinachomuuma zaidi mzee huyo.
Depay ambaye anafurahia maisha
Old Trafford hivi sasa alinukuriwa akisema, baada ya kutengwa na baba
yake amejikuta mjasiri na kwamba tattoo alizojichora mwilini zinampa
nguvu kuamini kwamba anaweza kufika mbali zaidi.
Comments
Post a Comment