Baba wa mtoto aliyekufa akataa hifadhi


 
Baba wa mtoto kutoka nchini Syria ambaye alikufa maji wiki hii na kuzua changamoto za kutaka kuchukuliwa hatua za kutatua suala la uhamiaji nchini syria anaripotiwa kukataa hatua ya Canada ya kumpa makao.

Tima Kurd, ambaye ni dadake Abdullah al Kurdi alisema, alimuambia kuwa anataka kusalia nchini Syria yaliko makaburi ya mkewe na wanawe wawili wa kiume ambao pia walikufa maji nje ya pwani ya Uturuki siku ya jumatano.
 
Image copyright Reuters
Image caption Baba na watoto wake waliokufa maji
Wote hao walizikwa nchini Syria siku ya Ijumaa
Picha za mwili wa mtoto huyo wa miaka mitatu katika ufuo wa Uturuki zilizua mjadala kuhusu hatma ya watu wanaokimbia mapigano nchini Syria.

Comments