BOMU LAUA POLISI 10 UTURUKI
Gari lisilopenya risasi liliharibiwa kabisa
Takriban polisi 10
wa Uturuki wameripotiwa kuuawa katika shambulio la bomu lililotegwa
ndani ya basi dogo mashariki mwa nchi hiyo .
Shambulio hilo limetokea siku mbili baada ya shambulio jingine dhidi ya magari ya kijeshi ya Uturuki kusini magharibi mwa nchi hiyo lililowauwa askari 16.
Wakati huo huo ndege za kijeshi za Uturuki zimefanya mashambiulizi zaid ya uvamizi dhidi ya ngome za PKK nchini Iraq.
Comments
Post a Comment